SHERIA NA MASHARTI YA KAWAIDA YA MATUMIZ

MAELEZO YA JUMLA

Ukurasa huu unafafanua sheria na masharti ya matumizi yanayotumika kwa watumiaji wote wa Intaneti wanaotembelea wavuti huo (hapa ndani "Wavuti").

Kama mtumiaji anayetembelea Wavuti, sheria na masharti haya ya matumizi yanakurejelea kama "Wewe", "Yako" na Yako".

Kwa kufikia na kutumia Wavuti huu, Unawajibika kamili kufuata sheria na masharti yafuatayo ya matumizi bila kuhifadhi.

Kwa sababu ya mabadiliko yanayoendelea katika Intaneti, hali za matumizi zinaweza kurekebishwa (ongezeko au uondoaji) wakati wowote na bila notisi. Kwa hivyo tunakushauri kushauriana nao mara kwa mara.

MALI YA KIAKILI

Wavuti huu unamilikiwa na Sanofi Kenya (hapa ndani itarejelewa kama "Kampuni") na unapangishwa na Sanofi Group.

Nyaraka, maudhui na vipengele vilivyoundwa kwa ajili ya Wavuti huo ni mali ya kipekee ya Kampuni au wahusika wengine walioidhinisha matumizi yao na Kampuni.

Wasilisho na kila vijenzi vyake (ikijumuisha alama za biashara, nembo na majina ya kikoa) vinavyoonekana kwenye Wavuti vimelindwa na sheria ya sasa ya mali ya kiakili na ni vya Kampuni na/au Sanofi Group au wahusika wengine walioidhinisha matumizi yao.

Hakuna nyenzo kutoka kwa Wavuti (ikijumuisha matini, nembo, michoro na picha) zinazoweza kunakiliwa, kuzalishwa upya, kubadilishwa, kupakuliwa, kuharibiwa, kuhamishwa au kusambazwa kwa njia yoyote, mzima au sehemu yake, bila ridhaa ya mapema, ya moja kwa moja na iliyoandikwa ya Kampuni. Matumizi yao yanategemea uidhinishaji.

Kama jambo la kipekee kwa vijenzi vya Wavuti vilivyo hapo juu (i) vinaweza kutumika kwa madhumuni ya taarifa kwa wanahabari na kufuata haki zilizoambatishwa kwa vijenzi hivi, ikijumuisha haki za mali ya kiakili, na (ii) nakala ya kijenzi kimoja au zaidi cha Wavuti kimeruhusiwa kwa matumizi Yako ya kibinafsi, mwenyewe na yasiyo ya kibiashara, na kwenye vifaa vyako vya kielektroniki vya kibinafsi.

Notisi inayofuata itaonekana kwenye nakala yoyote iliyoidhinishwa ya maudhui yote ya Wavuti au sehemu ya maudhui hayo: "HAKIMILIKI YA SANOFI-AVENTIS GROUP 2021 - HAKIMILIKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA"

Vipengele vya au vilivyopo katika Wavuti vilivyoruhusiwa kwa matumizi haviwezi kuharibiwa, kurekebishwa au kubadilishwa kwa njia yoyote. Matumizi yasiyoidhinishwa ya vipengele hivi husababisha ukiukaji.

Kampuni na Sanofi Group zina haki ya kuchukua hatua ya kisheria dhidi ya ukiukaji wowote wa haki zao za mali ya kiakili.

HALI YA TAARIFA

Madhumuni ya Wavuti huu ni kukusanya ridhaa ya kielektroniki ya wataalamu wa huduma ya afya.

Taarifa iliyotolewa kwenye Wavuti huu haitazingatiwa kama mwaliko wa kushauri au kununua dawa zilizozalishwa na Sanofi au yoyote kati ya mashirika yake madogo. Haitazingatiwa kama mwaliko wa kuwekeza na haitafasiriwa kama uombaji au toleo la umma na si sehemu ya ofa ya kujisajili, kununua au kuhusika katika hisa za Sanofi au thamani yoyote nyingine iliyowekwa na kutolewa na Sanofi na/au mashirika yake madogo.

WAJIBU WA WATUMIAJI WA WAVUTI

Ni jukumu lako la kuchukua tahadhari muhimu ili kuzuia maambukizo yoyote ua vifaa Vyako vya eletroniki vya kibinafsi kwa sababu ya matumizi ya Wavuti huu (ikijumuisha, japo haina kikomo kwa, "mtaliga" moja au zaidi, "Trojan horses” au "vimelea" vyovyote vingine).

Unawajibikia kutobadilisha mkondo wa Wavuti na madhumuni yake, au kuutumia kwa madhumuni haramu chini ya sheria ya Kenya au sheria yoyote nyingine ambayo Utahitaji kufuata. Isitoshe, Umepigwa marufuku dhidi ya kuruhusu au kuwezesha utofauti wowote haramu au matumizi ya Wavuti na mhusika mwingine.

Maoni au maudhui Unayoweza kuchapisha kwenye Wavuti yanafuatiliwa na Kampuni. Kampuni ina haki ya kuondoa maoni au maudhui yoyote inayoona kuwa yanakiuka sheria na kanuni zinazotumika, au ambayo Kampuni inaweza kuzingatia kama yasiyofaa (bila orodha hii kuwa na kikomo, hii inajumuisha maoni au maudhui yanayohusiana na nyenzo au tabia haramu, ya kuudhi, ya kudhihaki, yenye mambo machafu, yenye uchochezi, yenye filamu za ngono au ya unajisi inayoweza kuzingatiwa kama kosa au kusababisha dhima au ukiukaji wowote wa sheria). Kampuni pia ina haki ya kuwashtaki watumiaji wa Wavuti waliochapisha maoni au maudhui kama hayo, au kuruhusu kampuni yoyote katika Sanofi Group kuleta mashtaka kama hayo.

Maoni au maudhui Unayoweza kuchapisha kwenye Wavuti kimsingi hayaakisi maoni au mawazo ya Kampuni, wafanyakazi wake au mashirika yake mengine. Kampuni pia haiwezi kuthibitisha usahihi wa maoni au maudhui Unayoweza kuchapisha na haithibitishi, kuidhinisha au kuyaunga mkono. Katika tukio lolote, Kampuni haiwezi kuwajibikia uchapishaji wa maoni au maudhui kama hayo.

VIUNGO VYA WAVUTI MWINGINE

Wavuti unaweza kuwa na viungo vya wavuti wa wahusika wengine kwenye Intaneti. Si Kampuni wala Sanofi Group inayoweza kuwajibikia maudhui ya wavuti wa mhusika mwingine ambao huenda ulifikia kupitia Wavuti huu. Si Kampuni wala Sanofi Group ina njia yoyote ya kudhibiti maudhui ya wavuti kama huo wa wahusika wengine unasalia kuwa huru kabisa kwa Kampuni na Sanofi Group. Si Kampuni wala Sanofi Group inayoweza kuwajibikia ufikiaji wa wavuti kama huo wa mhusika mwingine. Zaidi ya hayo, uwepo wa kiungo kati ya Wavuti na wavuti wa mhusika mwingine kwa njia yoyote haimaanishi kuwa Kampuni au Sanofi Group imeidhinisha maudhui ya wavuti huu kwa njia yoyote, na hasa matumizi yanayoweza kutokana nao.

Wavuti wa mhusika mwingine unaweza kuwa na viungo vinavyokupeleka kwa Wavuti. Kiungo chochote kama hicho hakitasakinishwa bila kupata ridhaa ya mapema ya moja kwa moja na iliyoandikwa ya Kampuni. Katika tukio lolote, Kampuni haiwezi kuwajibikia (i) kutopatikana kwa wavuti wa nje kama huo, au (ii) asili na maudhui yao, ambayo Kampuni haikagui, kudhibiti au kuidhinisha.

TAARIFA YA SIRI NA YA KIBINAFSI

Kampuni inafahamu kabisa umuhimu wa faragha na ulinzi wa data ya kibinafsi katika kipindi cha kidijitali na imejitolea kuhakikisha kiwango kinachotosha cha ulinzi wa data kwa watu wote ambao Kampuni inafanya kazi nao.

Kando na data ya kibinafsi inayochakatwa kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha ambayo ni lazima usome na kukubali (tazama Sera ya Faragha ya Wavuti), taarifa yoyote kwa njia yoyote - nyaraka, data, michoro, maswali, mapendekezo, dhana, maoni au nyingine - unayowasiliana kwenye Wavuti kwa njia yoyote haitaonekana kuwa ya siri. Kwa sababu hiyo, uhamishaji wowote mdogo na Wewe hupatia Kampuni haki ya kutumia, kuzalisha upya, kusambaza, kurekebisha au kuhamisha taarifa hii ili kuchakata ombi Lako.

Tafadhali kumbuka kuwa majina ya mtumiaji na manenosiri ("Maelezo ya Muunganisho"), uliyopewa ili kuingia kwenye Wavuti, ni ya kibinafsi kwako na hayawezi kushirikiwa na mtu mwingine tena.

UWEKAJI KIKOMO KWA DHIMA

Kampuni inafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa taarifa iliyochapishwa kwenye Wavuti ni sahihi na ya hivi karibuni zaidi. Sanofi Group na Kampuni zina haki ya kurekebisha au kubadilisha maudhui ya Wavuti wakati wowote bila notisi. Hata hivyo, Kampuni haiwezi kukuhakikishia kuwa taarifa inayopatikana kwenye Wavuti ni ya kina, sahihi, kamili, ya kweli au ya hivi karibuni zaidi.

Kwa hiyo, na bila kujumuisha uharibifu wowote wa moja kwa moja unaotokana na uzembe au mwenendo mbaya kimakusudi kwenye sehemu yake, Kampuni inakataa dhima yoyote:

  • kwa muunganisho na makosa yoyote, mambo yasiyo wazi au kutoandika habari fulani kuhusu taarifa inayopatikana kwenye Wavuti;
  • inayoweza kutokana na uharibifu wowote kutoka kwa uvamizi wa ulaghai kwenye Wavuti na mhusika mwingine na inayoweza kuleta mabadiliko katika taarifa au vijenzi vinavyopatikana kwenye Wavuti;
  • kwa uharibifu wowote wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja, bila kujali vyanzo, asili, hali au matokeo, na ambao ungesababishwa kwa sababu ya (i) ufikiaji wowote wa Wavuti au kutowezekana kwa ufikiaji, (ii) matumizi ya Wavuti, ikijumuisha uharibifu wowote au mtaliga inayoweza kuathiri kompyuta Yako, na/au (iii) sifa ambayo Ungepatia taarifa yoyote moja kwa moja au si moja kwa moja kutoka kwa Wavuti. Aya hii inatumika, ikijumuisha katika visa ambapo Kampuni imeonywa dhidi ya uwezekano wa uharibifu kama huo.

Vijenzi vya Wavuti huo vimetolewa "kama ilivyo" bila uhakikisho wa aina yoyote, ama kabisa au wazi kabisa. Kampuni haitoi uhakikisho wa kabisa au wazi kabisa, unaohusika, bila kikomo, kwa thamani yao ya soko au umuhimu wa madhumuni yoyote.

UPATIKANAJI WA WAVUTI

Unakiri (i) kuwa haiwezekani kiufundi kutoa Wavuti bila matatizo yoyote na kuwa Kampuni haiwezi kuchukua wajibu wowote kwa hili; (ii) kuwa matatizo hayo yanaweza kufanya Wavuti kutopatikana kwa muda; na kuwa (iii) uendeshaji wa Wavuti unaweza kuathiriwa na hali na/au utendaji zaidi ya udhibiti wa Kampuni, kama vile, kwa mfano, viungo vya usambazaji na mawasilianoanga kati ya Wewe na Wavuti.

Kampuni na/au wasambazaji wake wanaweza, kwa wakati wowote, kwa muda au kwa kudumu kurekebisha au kukatisha ufikiaji wa Wavuti mzima au sehemu yake ili kuendesha ukarabati na/au kuboresha na/au kurekebisha Wavuti. Kampuni inakataa dhima yoyote ya uharibifu wowote unaoweza kutokana na mabadiliko katika, kusimamishwa au kusitishwa kwa ufikiaji wa Wavuti huo.

TAARIFA YA BIDHAA

Taarifa iliyo kwenye na kutangazwa kwenye Wavuti inajumuisha marejeleo ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja na bidhaa, mipango au huduma za Sanofi Group ambazo hazijapendekezwa au kupatikana katika nchi au maeneo fulani, au inayoweza kutolewa chini ya alama tofauti ya biashara, na inayoweza kufuata kanuni na hali tofauti za matumizi kulingana na nchi hiyo. Marejeleo ya aina hii hayafuati nia yoyote ya Sanofi Group ya kuuza bidhaa, mipango na huduma hizi katika nchi Yako. Tafadhali shauriana na kampuni au mshirika Wako wa kibiashara wa Sanofi kwa taarifa yoyote kuhusu bidhaa, mipango na huduma zinazopatikana katika eneo/nchi Yako.

UTOAJI WA KISHERIA

Wavuti na maudhui yake yapo chini ya sheria ya Kenya, na mgogoro wowote unaohusiana na sheria na masharti haya upo chini ya mamlaka kamili ya mahakama ya Kenya.

VIKWAZO VYA MATUMIZI

Mchapishaji wa Wavuti:

Sanofi Aventis Kenya Limited kampuni iliyo na dhima yenye kikomo na ofisi yake iliyosajiliwa ipo katika Crowne Plaza Annex, Orofa la 13 katika Barabara ya Longonot, Upper Hill, Nairobi Kenya

Mhariri Mkuu:

Mwelekezi wa uchapishaji ni Bw Peter Munyasi, Mwenyekiti wa Kitaifa wa Sanofi Aventis Kenya Limited Mkurugenzi mhariri ni Bi Maryanne Kariuki Mkuu wa Mawasiliano katika Sanofi-Aventis Kenya Limited

Upangishaji wa Wavuti:

Plusserver GmbH
Hohenzollernring 72
50672 Cologne
Ujerumani
Simu +49 2203 1045 3000