SERA YA FARAGHA

Sanofi imejitolea kamili kwa ulinzi wa data ya kibinafsi na itakupaia taarifa zote muhimu kuhusiana na inavyochakata data yako ya kibinafsi.

Utapata hapa chini maelezo yote muhimu kuhusu kuchakata data ya kibinafsi kwenye Wavuti huu. Tafadhali kumbuka kuwa maudhui ya sera hii ya faragha yanaweza kubadilika mara kwa mara, kwa mfano mabadiliko yakifanyika katika taratibu zetu kwa sababu ya sheria inayotumika. Ikiwa mabadiliko haya yana umuhimu wa wazi na huathiri haki au wajibu wako kulingana na ulinzi wa data yako ya kibinafsi (na kwa kiwango ambapo tuna njia ya kuwasiliana nawe), tutakuarifu kuhusu kisasisho hicho kwa njia inayofaa kutegemea taarifa ambayo huenda tumekusanya.

Hata hivyo, tunakushauri uangalie ukurasa huu wa sera ya faragha mara kwa mara ili kupata visasisho.

NANI ANAWAJIBIKIA UCHAKATAJI WA DATA YA KIBINAFSI KWENYE WAVUTI HUU?

Sanofi Ethiopia inawajibikia kuchakata data ya kibinafsi ya watu wanaotumia Wavuti huu na kwa hivyo inafanya kazi kama Mdhibiti wa Data:

Sanofi Aventis Kenya Limited,
Crowne Plaza Annex, 13th Floor,
Longonot Road,
Upper Hill,
Nairobi,
Kenya

Sanofi Aventis Kenya Limited kampuni iliyo na dhima yenye kikomo na ofisi yake iliyosajiliwa ipo katika Crowne Plaza Annex, Orofa la 13 katika Barabara ya Longonot, Upper Hill, Nairobi, Kenya.

KIKUMBUSHO: UCHAKATAJI WA DATA YA KIBINAFSI NI NINI?

Kwa madhumuni ya sera hii ya faragha, data ya kibinafsi inafaa kukusanywa kama taarifa yoyote inayohusiana na mtu aliyetambuliwa au anayeweza kutambuliwa, iliyochakatwa na Sanofi kama sehemu ya malengo na madhumuni yaliyofafanuliwa katika Sera hii ya Faragha.

Ili kufafanua chochote unachoweza kuelewa vibaya, hii ni taarifa yoyote inayohusiana na mtu. Data hii ya kibinafsi inaweza, kwa mfano, kuchukua hali ya:

 • Taarifa msingi ya utambulisho kama vile jina lako au tarehe yako ya kuzaliwa;
 • Taarifa inayoweza kupewa sifa za moja kwa moja au si moja kwa moja nawe, kama vile ujumbe kwenye mtandao wa kijamii;
 • Taarifa inayoweza kuhusishwa nawe au kuhusishwa na kifaa chako, kama vile anwani ya IP (yaani, anwani ya mtandao ya kifaa chako);

Kwa mujibu huu, dhana ya "kuchakata" inarejelea hatua yoyote inayochukuliwa kwenye data yako ya kibinafsi, kwa mfano:

 • ukusanyaji
 • uhifadhi
 • ufikiaji
 • uchanganuzi
 • ufutaji

WAVUTI HUU HUKUSANYA DATA GANI YA KIBINAFSI

Katika utendaji wake, Wavuti huu unaweza kukusanya kategoria zifuatazo za data ya kibinafsi:

 • Data ya utambulisho: taarifa yoyote ambayo huruhusu utambulisho wako, moja kwa moja au si moja kwa moja, kama vile jina lako au taarifa ya mawasiliano (anwani, anwani ya barua pepe, nambari ya simu), aina ya kazi yako, biashara yako
 • Ujumbe: unaweza kututumia maulizo kwa kutumia Wavuti huu
 • Taarifa ya biashara
 • Data ya muunganisho: taarifa yoyote kuhusu muunganisho wako na ufikiaji wa Wavuti huu (mfano aina ya kompyuta na kivinjari kilichotumika, saa ya muunganisho wako, anwani ya IP, kurasa ulizotazama, historia ya kuvinjari)
 • Data ya eneo: Taarifa inayoweza kutolewa na kompyuta na kivinjari chako kuhusu eneo lako ukiruhusu taarifa hii kushirikiwa na Sanofi
 • Data inayohusiana na, na data inayoweza kukusanywa kwa vidakuzi: Kwa taarifa zaidi kuhusu vidakuzi, tafadhali soma yanayofuata
 • Katika hali maalum, Sanofi inaweza kuchakata taarifa inayohusiana na maoni ya kifalsafa, kisiasa na kidini, uanachama wa muungano, mwelekeo wa kingono, afya, asilia ya kirangi au kikabila: Sanofi itachakata tu kategoria hizi za data ya kibinafsi, zinazozingatiwa kama data "nyeti" ya kibinafsi au "kategoria maalum" ya data ya kibinafsi, ikiwa hii itaidhinishwa vizuri chini ya sheria zilizopo za ulinzi wa data. Hasa, Sanofi itachakata tu taarifa hii ikiwa imepata ridhaa yako dhahiri na maalum ya kufanya hivyo.

WAVUTI HUUHUKUSANYADATA YA KIBINAFSI KWA MADHUMUNI GANI?

Uchakataji wowote wa data ya kibinafsi lazima ufanywe kwa madhumuni yaliyofafanuliwa. Kwa mujibu huu, ukusanyaji na uchakataji wa data ya kibinafsi kwenye Wavuti huu unafanywa kwa madhumuni yafuatayo:

 • Kukuruhusu kuvinjari wavuti huu
 • Kukupatia ufikiaji wa huduma za mtandaoni, programu na majukwaa: kudhibiti akaunti zako mtandaoni
 • Kugeuza uzoefu wako wa kuvinjari ili uwe wa kukufaa: wakati wa kutumia huduma zetu, hakikisha kuwa huduma zetu zimewasilishwa kwa njia bora kwako, fahamu mapendeleo yako ya kitaalamu na ya kibinafsi katika maudhui, bidhaa na huduma zetu au maudhui mengine na kufanya maudhui yetu yafuatilie mahitaji na mapendeleo yako; kukutanguliza kwa bidhaa na ofa ulizoandaliwa
 • Kuboresha bidhaa na huduma zetu: tambua mielekeo ya matumizi na uunde bidhaa na huduma mpya; fahamu jinsi wewe na kifaa chako huingiliana na huduma zetu; dhibiti na utatue wasiwasi wa usalama; tambua ufaafu wa kampeni zetu za matangazo, fanya uchunguzi
 • Kuturuhusu kuwasiliana nawe: jibu maombi au maulizio yako; toa msaada kwa bidhaa na huduma; kukupatia taarifa muhimu, taarifa ya utawala, arifa zinazohitajika na nyenzo za matangazo; kukutumia habari na taarifa kuhusu bidhaa, huduma, chapa, uendeshaji wetu; panga na kudhibiti matukio na mikutano ya kitaalamu, ikijumuisha ushiriki wako katika matukio kama hayo.

WAVUTI HUU HUCHAKATA DATA YAKO YA KIBINAFSI KWA MSINGI UPI?

Kwa madhumuni ya Wavuti huu, data yako ya kibinafsi huchakatwa tu kwa msingi wa:

 • Ridhaa yako ya awal: (i) pahali ambapo umeonyesha dhahiri uidhinishaji wako wa Sanofi kuchakata data yako ya kibinafsi. Katika matumizi, hii mara nyingi humaanisha kuwa Sanofi itakuomba kusaini waraka, au kujaza fomu ya mtandaoni ya kuingia au kufuata utaratibu wowote muhimu wa kukuruhusu kuwa na ufahamu kabisa na kisha ama kukubali au kukataa kwa uwazi uchakataji wa data ya kibinafsi inayotazamiwa. (ii) Kwa kuvinjari wavuti huu na, ikiwa ni muhimu, kutoa ridhaa kwa uchakataji wa data yako ya kibinafsi kwa kutumia vidakuzi (kwa mujibu wa sera yetu ya kidakuzi hapa chini).
 • Uhusiano wa kimkataba kati yako na Sanofi: katika hali hii, uchakataji wa data yako ya kibinafsi huwa muhimu ili kukamilisha au kutekeleza mkataba huo; hii inamaanisha kuwa ikiwa hutaki Sanofi ichakate data yako ya kibinafsi katika muktadha huu, Sanofi inaweza au itahitajika kukataa kuingia katika mkataba kama huo na wewe ama haitaweza kutoa bidhaa au huduma zilizopo chini ya mkataba huu.
 • "Matamanio halali" ya Sanofi ndani ya maana ya sheria husika za ulinzi wa data. Katika hali hii, Sanofi inazingatia haki na matamanio yako ya kimsingi katika kutambua kama uchakataji huo ni halali na wa kisheria.

HDATA YA KIBINAFSI INAYOKUSANYWA KWENYE WAVUTI HUU HUHIFADHIWA KWA MUDA UPI?

Sanofi haitaweka data yako ya kibinafsi zaidi ya inavyohitajika. Sanofi itahifadhi tu data yako ya kibinafsi kwa kipindi muhimu kufanikisha madhumuni yaliyotajwa katika Sera hii. Sanofi itakuambia kipindi cha muda hasa husika kupitia Mitajo ya Taarifa inayohusiana na hapo.

Kwa kupunguza makali ya kanuni, Sanofi inaweza kuhitajika kuhifadhi Data yako ya Kibinafsi kwa kipindi kirefu, kwa mujibu wa jambo lililoidhinishwa au kupendekezwa na sheria husika, au katika kiwango ambacho ni muhimu kulinda haki na mapendeleo yake.

Kuhusiana na data kuhusu na data inayoweza kukusanywa kwa vidakuzi: tafadhali rejelea sera kuhusu matumizi ya vidakuzi.

ALIYENAUFIKIAJI WADATA YA KIBINAFSI

Sanofi inaweza kuhamisha data yako ya kibinafsi ndani (yaani kwa mashirika mengine ya Sanofi) na/au nje kwa wahusika wengine wanaotoa huduma kwa ajili ya:

 • usimamizi wa akaunti yako
 • kutambua ufikiaji wa Wavuti huo
 • kuboresha na kubinafsisha Kituo na bidhaa, huduma zetu na shughuli yetu kwa jumla
 • kuingiliana nawe ili kutatua ombi au malalamiko yoyote
 • kufahamu vyema matamanio na mapendeleo yako, kuboresha njia zetu za mawasiliano na mwingiliano nawe
 • kukutumia mawasiliano na taarifa nyingine tunayodhani inaweza kuwa muhimu kwako au uliyotuomba

Pahali ambapo uhamishaji huu wa data ya kibinafsi ndani au nje huhusisha uhamishaji wa data ya kibinafsi kwa nchi inayotoa ulinzi wa chini wa data ya kibinafsi kuliko ule unaotolewa kwa kawaida katika nchi yako, Sanofi itahakikisha kuwa kiwango cha ulinzi kinachotosha kimetolewa kwa data yako ya kibinafsi, kwa kutekeleza ulinzi wa kutosha kama vile vifungu vya mkataba wa Kiwango cha Ulaya na kanuni za Sanofi za kibiashara za kufungamanisha, au kwa kuomba ridhaa yako dhahiri ya mapema.

HAKI ZAKO: SANOFI ITAHAKIKISHA KUWA UNAWEZA KUTUMIAHAKI ZAKOKUHUSUDATA YAKO YA KIBINAFSI

Unaweza kutumia haki zako ilivyotolewa na sheria zinazotumika za ulinzi wa data.

Kwa kusudi hili, Sanofi inakufahamisha kuwa una haki ya:

 • kufikia, kwa ombi sahili, data yako ya kibinafsi - ambapo katika hali hiyo unaweza kupokea nakala ya data hii (ikiwa uliomba), isipokuwa kama unaweza kupata data hiyo moja kwa moja, kwa mfano katika akaunti yako ya kibinafsi;
 • kupata marekebisho ya data yako ya kibinafsi ikiwa si sahihi, haijakamilika au imepitwa na muda;
 • kupata ufutaji wa data yako ya kibinafsi katika hali zilizopo kwenye sheria iliyopo ya ulinzi wa data ("haki ya kusahauliwa");
 • kuondoa ridhaa yako ya uchakataji wa data yako ya kibinafsi bila kuathiri uhalali wa uchakataji huo, ikiwa data yako ya kibinafsi imekusanywa na kuchakatwa kwa msingi wa ridhaa yako;
 • kukataa uchakataji wa data yako ya kibinafsi, wakati hizi zimekusanywa na kuchakatwa kwa msingi wa mapendeleo halali ya Sanofi, katika hali ambapo unahitaji kuhalalisha ombi lako kwa kutuambia hali yako hasa;
 • kuomba uwekaji kikomo kwenye uchakataji wa data ya kibinafsi katika hali zinazoweza kutabiriwa chini ya sheria iliyopo ya ulinzi wa data;
 • kupokeadata yako ya kibinafsiili ziweze kuhamishwa kutoka kwa Sanofi kwenda kwa mhusika mwingine au data yako ya kibinafsi kuhamishwa moja kwa moja na Sanofi kwenda kwa wahusika wengine unaowapenda, panapowezekana kiufundi (haki ya usafirishaji wa data inaruhusiwa tu wakati wa kuchakata kutegemea ridhaa yako)

Ikiwa unataka kutumia yoyote kati ya haki hizi, tafadhali wasiliana nasi kwa njia iliyoonyeshwa katika kitengo cha "Jinsi ya kuwasiliana nasi" hapo chini. Kisha tutachukua hatua muhimu ili kukujibu haraka iwezekanavyo.

Unaweza pia kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka hodari ya ulinzi wa data kuhusu uchakataji wa data yako ya kibinafsi. Ijapokuwa tunapendekeza kuwa uwasiliane nasi mapema, ikiwa unataka kutumia haki hii, unafaa kuwasiliana moja kwa moja na mamlaka husika ya ulinzi wa data.

JINSI YA KUWASILIANA NASI

Unaweza kutuma maswali au maombi yote kuhusu jinsi Sanofi hutumia data yako ya kibinafsi kwa kututumia barua pepe kupitia anwani inayofuata: Sanofi Aventis Kenya Limited,
Crowne Plaza Annex, 13th Floor,
Longonot Road,
Upper Hill,
Nairobi,
Kenya